Klabu ya soka ya Young Africans SC imeingia mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF unaolenga kuongeza uelewa kwa Umma kuhusu Chanjo ya UVIKO-19 na uhamasishaji kuhusu virusi vya EBOLA.
Mtendaji mkuu wa Young Africans SC Andre Mtine alisema leo ni siku ya Kihistoria kwa Klabu yetu kuingia mkataba mkubwa na shirika kubwa duniani.
Mnamo Septemba 20, 2022 serikali ya Uganda ilitangaza mlipuko wa virusi vya Ebola katika eneo la magharibi mwa nchi.
Ni heshima kubwa kuingia mkataba na UMOJA WA MATAIFA. Ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa Vilabu vya hapa Afrika Mashariki. Ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya Klabu yetu ya kusaidia jamii.
“Tunajulikana kama timu ya Wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Wananchi,” Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said
0 Comments