Mama mmoja raia wa Nigeria ameshangaa kwamba mwanawe ambaye hula chakula kidogo nyumbani hurejea kutoka shuleni kila siku na chupa tupu.Mama huyo aliandika kupitia Twitter kuwa Ili kupata uhakika kuhusu mawazo yake, alimpeleka mtoto wake shuleni akiwa na chakula ambacho huwa hakipendi na bado alirudi kikiwa kimeisha Mwanamke huyo alisema hatimaye aligundua ujanja wa walimu kuwa walikuwa wakila mlo wote wa mwanae.
Mwanamke huyo alisema kila mara alishuku kuwa kuna mtu alikuwa akila chakula cha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili ambaye huwa anabeba hotpot lililojaa mlo.
"Nilimpa ndizi mbichi zilizochemshwa na mchuzi wa mboga! Nikijua vizuri mwanangu anachukia ndizi mbichi. Nilishtuka aliporejea nyumbani na chupa tupu. "Kwa hivyo ulikuwa mtihani, kwa sababu hotpot lake ni kubwa na kwa mtoto wa miaka 2 hawezi kula sana. Nilijua kuwa kuna kitu hakikuwa sawa! Angalau anapaswa kurejea nyumbani na chakula alichobakisha. Ilibidi nitumie ujanja ndipo nijue kile kilikuwa kinaendelea na sasa majibu nimepata bayana. Hapo ndipo nilijua walimu wake wanakula vizuri!"
Thank you 😂one time I packaged boiled unripe plaintain and egg/vegetable sauce ! Knowing fully well my son hates unripe plantain … Lo and behold brethren 😂he came back with an empty Flask… that was when I knew this teachers are eating good !
— officialDebbiecruz# (@Dcounty93) October 12, 2022
0 Comments